Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanaopinga ubaguzi wasinyamazishwe:UM

Wanaopinga ubaguzi wasinyamazishwe:UM

Kundi la wataalamu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa watoa wito kwa mataifa kuchukua hatua dhidhi ya kuendelea kulengwa kwa wanaotetea haki za binadamu hali ambayo imesababisha vifo vya viongozi wa kijamii, mawakili , waandishi wa habari , wanaotetea wanawake na wengine wanaofanya jitihada za kumaliza ubaguzi na ukiukaji wa sheria.

Kundi hilo limezitaka nchi kutekeleza yale yanayopendekezwa na watetezi wa haki na pia kuwahakikishia usalama. Aidha wamezitaka nchi kuheshimu haki za wanaotetea haki za binadamu zikiwemo haki za kuzungumza na kukusanyika . Kwa maoni yao kila nchi inahitaji kuhakikisha sera zake zinaambata na viwango vya kimataifa katika masuala ya kulinda haki za binadamu.