Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matokeo ya uchaguzi yazua ghasia Haiti

Matokeo ya uchaguzi yazua ghasia Haiti

Maandamano pamoja na milio ya riasasi imeripotiwa kwenye mji wa Port-au-Prince nchini Haiti baada ya maafisa wa uchaguzi kutangaza kuwa kutakuwa na duru ya pili ya uchaguzi wa urais.

Aliyekuwa mke wa Rais wa nchi hiyo  Mirlande Manigat, atashiriki katika duru ya pili ya uchaguzi mwezi Januari mwaka ujao akipambana na Jude Celestian ambaye ni mgombea wa chama tawala. Wakati huo huo shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema kuwa hadi sasa ugonjwa wa kipindu pindu umewaua zaidi ya watu 2,100 nchini Haiti. OCHA linasema kuwa kuwapa watu habari kuhusu jinsi ya kuepukana na ugonjwa huo na mahala wanaweza kupata matibabu bado ni changamoto kubwa.