Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ununuzi wa chakula na uhaba wa maji ni chanzo cha uhaba wa chakula katika nchi za Mashariki ya Karibu:FAO

Ununuzi wa chakula na uhaba wa maji ni chanzo cha uhaba wa chakula katika nchi za Mashariki ya Karibu:FAO

Mkurugenzi wa shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO Jacques Diouf amesema kuwa kuongezeka kwa idadi ya watu kwenye nchi za mashariki ya karibu hakuambatani na kuzalishwa kwa vyakula hali ambayo inayafanya mataifa ya eno hilo kutegemea ununuzi wa vyakula.

Kwa ujumla idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa na utapiamlo katika nchi za mashariki ya karibu inakadiriwa kuwa watu milioni 37. Akiongea kwenye mkutano wa nchi za mashariki ya karibu unaondelea mjini Khartoum nchini Sudan Diouf amesema kuwa iwapo mazao ya vyakula yameongezeka katika nchi zingine lakini bado uzalishaji wa ujumla ni wa chini. Amesema kuwa ili kukabiliana na hali hiyo inahitaji kuwepo uwekezaji katika sekta ya kilimo.