Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa kilimo cha mboga na matunda wakutana Senegal

Wataalamu wa kilimo cha mboga na matunda wakutana Senegal

Naibu katibu mkuu wa shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO amesema kuwa wanaohusika na kutoa mipangilio ya miji wanastahili kujumuisha kilimo cha matunda na mboga kwenye mipangilio hiyo kama moja njia ya kukabiliana na changamoto za kulisha idadi ya wakaazi wa mijini inayondelea kuongezeka kila siku.

Modibo Traore anasema kuwa zaidi ya nusu ya watu wote duniani kwa sasa wanaishi mijini wakati bilioni moja kati yao wakiishi sehemu za mabanda hususan barani Afrika , Asia na Amerika Kusini na huenda idadi hiyo ikaongezeka zaidi ifikapo mwaka 2050 . George Njogopa na taarifa kamili:

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)