Ulaya yatakiwa kuongoza misaada kwa nchi maskini:BAN
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa muungano wa ulaya unaweza kuongoza kuwepo kwa ushirikiano wa kimaendeleo katika kusaidia nchi maskini.
Juma lililiopita Ban alitoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano katika masuala kadha yakiwemo ya usalama kati ya Umoja wa Mataifa na shirika la usalama barani ulaya lililo na wanachama 56 kutoka Marekani kwenda ulaya na kati kati mwa bara Asia.