Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amuunga mkono mwakilishi wake kuhusu uchaguzi Ivory Coast

Ban amuunga mkono mwakilishi wake kuhusu uchaguzi Ivory Coast

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa taarifa leo kuuunga mkono msimamo wa mwakilishi wake nchini Ivory Coast kuhusu matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi wa Rais.

Bwana Y.J Choi alithibitisha na kukubaliana na matokeo ya uchaguzi wa Novemba 28 yaliyotangazwa jana Desemba pili na rais wa tume huru ya uchaguzi nchini humo na kusema mgombea wa uchaguzi wa upinzani Assane Ouattara ameshinda duru hiyo ya pili ya uchaguzi.

Katibu Mkuu amewapongeza watu wa Ivory Coast kwa ushiriki wao kwenye uchaguzi huo na amempongeza bwana Ouattara wa chama cha RHDP kwa kuchaguliwa kwake, amemtaka aendeleze juhudi za kupatikana amani ya kudumu, utulivu na maridhiano nchini humo.

Ban pia amemtaka Rais Laurent Bagbo anayeondoka madarakani kutekeleza wajibu wake kwa maslahi ya nchi na kushiriki kuhakikisha amani katika kipindi cha mpito cha kisiasa nchini humo.Hata hivyo hali bado ni tete baada ya mahakama ya katika kubadili matokeo na kumtangaza Laurent Bagbo ndiye mshindi tangazo ambalo linapindua uamuzi wa tume huru ya uchaguzi.