Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katika siku ya walemavu duniani UM unataka nchi ziwasaidie zaidi walemavu

Katika siku ya walemavu duniani UM unataka nchi ziwasaidie zaidi walemavu

Katika kuadimisha siku ya kimataifa ya walemavu kauli mbiu ya mwaka huu ni kutimiza ahadi, na kuwashirikisha walemavu katika malengo ya maendeleo ya milenia.

Akitoa ujum,be maalumu hii leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ulemavu kwa kiasi kikubwa unahusishwa na umasikini, kwani watu wenye ulemavu ni asilimia 20 ya watu wote masikini wanaoishi kwenye nchi zinazoendelea.

Ban amepongeza msimamo juhudi zinazoonyeshwa na watu wenye ulemavu na ametoa wito kwa serikali kujitahidi kuwasaidia zaidi watu wenye ulemavu.Amesema tutambue kwamba vita dhidi ya umasikini , maradhi na ubaguzi hatutovishinda kama hakutokuwa na sheria, sera na mipango ya kuwawezesha walemavu.

Chishaya Emmanuel ni mlemavu kutoka Burundi anasema kwa kiasi kikubwa walemavu bado hawathaminiwi wala kupewa haki.

(SAUTI YA CHISHAJA EMMANUEL)