Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunaupungufu mkubwa wa fedha kuisaidia DR Congo:OCHA

Tunaupungufu mkubwa wa fedha kuisaidia DR Congo:OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema operesheni zake za misaada nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zinakabiliwa na matatizo makubwa ya kifedha.

Kwa mujibu wa shirika hilo katika msaada wote unaohitajika wa asilimia 100 ni asilimia 59 tuu iliyopatikana kufikia leo Novemba 30, ambao ni dola milioni 489 kati ya dola milioni 827 zilizoombwa.

OCHA inasema watoto wapatao 200,000 ambao wanaugua utapia mlo hawajapata msaada unaohitajika, huku wengine 180,000 walio na umri wa mwaka mmoja hawajapata chanjo na zaidi ya watoto laki moja wa chini ya umri wa miaka mitano wako katika hatari ya kupata malaria.

Kwa watu wazima na wasichana wapatao 38,000 amao ni waathirika wa ubakaji wako katika hatitahi ya kupata ukimwi kutokana na ukosefu wa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo. Elizabeth Byrs ni msemaji wa OCHA.

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)