Maonyesho ya mandeleo ya nchi za kusini mwa ulaya yakamilika Geneva

26 Novemba 2010

Maonyesho kimaendeleo ya juma moja ya nchi za kusini mwa Ulaya yaliyokuwa yamendaliwa mjini Geneva yamekamilika hii leo huku washirikia wakionyesha na kubadilishana zaidi ya suluhu 100 ambazo zinaweza kusaidia kutimizwa kwa maelngo ya maendeleo ya millenia.

Akiongea wakati wa kumalizika kwa mkutano huo mkuu wa shirika la afya duniani WHO Margaret Chan amesema kuwa mbinu za keleta maendeleo ni lazima zitegemee suluhu za nchi zenyewe. Naye rais wa mkutano wa 65 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Joseph Deiss pia alizungumzia umuhimu wa kubadilisha uvumbuzi kama moja ya njia kuimarisha maeendeleo. Prudence Mabele mmoja wa wanawake wa kwanza nchini Afrika Kusini kujitokeza wazi kuwa alikuwa na virusi vya ukimwi alihudhuria maonyesho hayo na leo hii yeye ni mwanaharakati maarufu wa ugonjwa wa ukimwi. Alipata kuzumgumza na Ben Malor wa Redio ya UM kabla ya kumalizika kwa maonyesho hayo.

(SAUTI YA PRUDENCE MABELE)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter