Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya UM aunga mkono kutekelezwa kwa mkataba ya kutoweka kwa watu

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya UM aunga mkono kutekelezwa kwa mkataba ya kutoweka kwa watu

Mkuu wa tume ya Umoja wa Kimataifa ya haki za binadamu Navi Pillay ameunga mkono kuanza kutumika kwa mkataba mpya wa haki za binadamu wa kutokomeza kutoweka kwa lazima na kuwachukulia wahusika hatua na pia kuwalinda waathiriwa.

Makubalino hayo yanaanza kutumika rasmi siku thalathini baada ya Iraq kuwa taifa la ishirini kuyaidhinisha. Mkataba huo unaeleza kuwa hakuna hali ambayo itasababisha kutoweka kwa mtu iwe vita , hatari ya kutokea kwa vita , msukosuko wa kisiasa au hali yoyote ile ya dharura. Pia unaeleza kuwa hakuna yeyote ambaye atawekwa kwenye kizuizi cha kisiri na mataifa wanachama ni lazima kumchukulia hatua yeyote anayetenda , kuamuru au kujaribu kuhusika na kutoweka kwa lazima kwa watu. Makubalino hayo yalioyoafikiwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2006 yalisubiri kuidhinishwa na mataifa 20 kabla ya kuanza kutumika. Mataifa mengine 70 yamechukua hatua za kuyatia sahihi ikiwa ni ishara kuwa huenda yakayaidhinisha katika siku za usoni.