Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zatakiwa kushughulikia uovu wanaotendewa watu wanaosafirishwa kiharamu

Nchi zatakiwa kushughulikia uovu wanaotendewa watu wanaosafirishwa kiharamu

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu usafirisha haramu wa watu Jay Ngozi Ezeilo amezitaka nchi zote watakotoka watu wanaosafirishwa kiharamu , wanakopitishwa au kufikishwa kuhakikisha wahusika wamepata haki zao.

Akiongea kwenye mkutano wa wataalamu wanaopinga usafirishaji haramu wa watu mjini Bratislava nchini Slovakia Ezeilo amesema kuwa watu waliosafirishwa kiharamu ni lazima wapate utulivu na hata kufidiwa kutokana na magumu ambayo wamepitia. Bi Ezeilo alisisitiza kuwa haki ya kupata habari, uwakilishi wa kisheria na hali yao ya kuishi ni huduma muhimu wanazostahili kupata watu waliosafirishwa kiharamu ili kuwahakikishia haki yao ya kupata utulivu. Mtaalamu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa nchi wanakotoka , kupitia na nchi zao za mwisho zina jukumu la kuwahakikishia utulivu watu waliosafirishwa kiharamu.