Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uandikishaji kura ya maoni Kaskazini mwa Sudan hauridhishi:UM

Uandikishaji kura ya maoni Kaskazini mwa Sudan hauridhishi:UM

Kumekuwa na mwamko mgodo wa wananchi wa Sudan Kusin ambao wanaishi upande wa pili yaani Sudan Kaskani wanaojitokeza kujiandikisha kwenye daftari la upigaji kura kwa ajili ya kura ya maoni itayofanyika January mwakani.

Mwenyekiti anayeongoza jopo lilitoteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kufuatilia kura hiyo ya maoni Bwana Benjamin Mkapa amesema kuwa hali hiyo imesababishwa na mambo kadhaa ikiwemo wananchi hao hawakuhamasishwa vyakutosha.

Bwana Mkapa ambaye pia ni rais wa zamani wa Tanzania ameeleza kuwa hali ya wasiwasi na kutokuwa na uhakika juu ya majaliwa ya baadaye huenda pia imesabisha wananchi hao washindwe kujitokeza.

Wananchi hao wa Sudan Kusin wanatazamiwa kupiga kura hiyo ya maoni January 9 kura ambayo itaamua kama eneo hilo litajitenga kutoka Sudan na kuwa taifa linalojitegemea. Wananchi wa jimbo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Abyei nao watapiga kura ambayo itamua wakae upande upo kati ya sehemu hizo mbili.

Kura hiyo ni utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa mwaka 2005 ambayo yalimaliza miongo kadhaa ya uhasama kati ya Kusin na Kaskani.