Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kimataifa ya watoto inaadhimishwa Iraq

Siku ya kimataifa ya watoto inaadhimishwa Iraq

Majimbo yote ya Iraq jana Jumapili yameanza siku kumi za maadhimisho ya sherehe za siku ya kimataifa ya watoto ambapo tarehe 21 Novemba ni siku ya maadhimisho ya mkataba wa haki za mtoto.

Viongozi wa serikali, kijamii na maelfu ya watoto wanatarajiwa kushiriki katika sherehe za mwaka huu. Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Iraq Sikander Khan amewatolea wito Wairaq wote kuwa msitari wa mbele kulinda na kuheshimu haki za watoto.

Amesema endapo sisi wote, magavana, na wadau wa kitaifa na kimataifa ktutaanza kuwekeza katika watoto wa Iraq basi tunaona sio tuu watoto wakilindwa n kuwa na afya nzuri bali pia tutaiona Iraq ambayo itarejea katika hali ya amani, utulivu na kuwa taifa lenye maendeleo.