Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya WHO inataka zichukuliwe hatua kuhakikisha kila mtu anamudu huduma za afya

Ripoti ya WHO inataka zichukuliwe hatua kuhakikisha kila mtu anamudu huduma za afya

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa gharama za matibabu zinaendelea kuwa ghali na kusababisha mamilioni ya watu na hata kutoka mataifa yaliyostawi kuwa maskini.

WHO inasema kupanda kwa gharama za matibabu kunachochewa na idadi kubwa ya watu wazee, idadi kubwa ya visa vya magonjwa sugu na kuweo matibabu ya kisasa ya gharama ya juu. Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka huu ya afya, WHO inatoa wito kwa serikali kutenga fedha zaidi kwa sekta ili kuiwawesesha watu zaidi kupata matibabu. David Evans ni mkurugenzi wa masuala ya ufadhili wa afya wa WHO.

(SAUTI YA DR DAVID EVANS )

WHO inatoa wito kwa jamii ya kimataifa kusaidia nchi zenye kipato cha chini na cha wastani katika juhudi zao za kutoa huduma za afya ikisema kuwa gharama za matibabu zinawafanya maskini watu milioni mia moja kila mwaka duniani.