Skip to main content

Kesi ya Jean Pierre Bemba imeaanza mahakama ya ICC

Kesi ya Jean Pierre Bemba imeaanza mahakama ya ICC

Kesi ya aliyekuwa kiongozi wa kundi la waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean Pierre Bemba imeanza kusikilizwa leo kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC mjini the Hague Uholanzi.

Bemba anakabiliwa na mashitaka matato ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Kesi hiyo inahusiana na vitendo vilivyotekelezwa na waasi wa kundi lake la MLC dhidi ya raia wan chi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kati ya mwaka 2002 na 2003.

Bemba alikuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na ni miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu barani Afrika kufikishwa katika mahakama hiyo. Upande wa mashitaka unasema alishindwa kudhibiti vikosi vyake wakati vilipotekeleza uhalifu huo.

Bemba mwenye umri wa miaka 48 amekana mashitaka yote yanayomkabili, mawili ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na matatu ya uhalifu wa kivita. Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea kwa miezi kadhaa kabla ya hukumu kutolewa.