Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yataka uvuvi haramu duniani uchunguzwe

FAO yataka uvuvi haramu duniani uchunguzwe

Kama njia ya kumaliza uvuvi haramu duniani shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limekubali kuchunguza mipangilio ya kutekelezwa na kuwekwa kwa kumbukumbu kwa vyombo vya uvuvi vinavyosafirisha na kuhifadhi na vile vinavyosambaza samaki.

Mapendekezo hayo yatawasilishwa mbele ya kamati ya shirika la FAO inayohusika na uvuvi Januari mwakani ili kuyaidhinisha kama moja ya juhudi ya kuokoa na kuinua hali ya maisha ya mamilioni ya watu wanaotegemea sekta ya uvuvi. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Shirika hilo limesema kuwa linakusudia kuboresha hali ya uwazi na ukweli kwenye sekta hiyo ya samaki katika uso wa dunia ikiwa ni hatua ya kwanza ya kukabiliana na vitendo hivyo vya uvuvi haramu. Vitendo vya uvuvi haramu vimeendelea kuongezeka katika maeneo mbalimbali na kukosekana kwa mbinu madhubuti ya kukabili hali hiyo imezidi kuongeza kasi ya vitendo hivyo.

Hata hivyo FAO imesema itaanza kufanya kazi kwa ushirikiano dhati na mamlaka mbalimbali hatua ambayo itaongeza hali ya uwazi na ukweli kwenye kufuatilia vyombo vya usafiri vinavyodhaniwa kuendesha shughuli za uvuvi harama.