Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bara la Afrika halifaidiki na mali asili yake:UNCTAD

Bara la Afrika halifaidiki na mali asili yake:UNCTAD

Mkutano wa 14 wa UNCTAD kuhusu mafuta, gesi, Madini, biashara na masuala ya fedha Afrika utafanyika Sao Tome , katika visiwa vya Sao Tome na Principle.

Mkutano huo utakaoanza Novemba 21 hadi 25 utakjikita katika upatikanaji wa faida kutokana na mali asili katika kuleta maendeleo ya bara hilo. Hivi sasa faida kubwa ya mali asili hiyo inapotelea mikononi mwa makampuni ya kigeni katika hatua mbalimbali hasa katika madini.

Mali asili za Afrika zinawavutia wawekezaji wengi wa kigeni, suala ambalo linasababisha faida ya uwekezaji huo kuhamia ughaibuni na kunufaisha viwanda vya kigeni. Jayson Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)

 Mara nyingi makampuni yanayohusika hayana uhusiano wa moja kwa moja na uchumi wa nchi ambapo yanaendesha shughuli zake. Wataalamu wanasema kuwa inazihitaji nchi za kiafrika kuwa na sekta na sera na pia kuchunguza masuala kama hayo.

Mkutano huo utatafuta sera mwafaka na uchuzi kutoka sehemu zingine za ulimwengu kuhusu ni njia zipi sekta kama hizo zinaweza kuchangia kuinuka kwa uchumi wa barani Afrika. Mkutano huo utawaleta pamoja maafisa kutoka nchi za Afrika wakiwemo mawaziri kumi wa kawi , mawaziri wanaohusika na uchimbaji wa madini na wa uchumi na maafisa kutoka kwa makambuni ya mafuta.

Pia mkutano huo unatarajiwa kuwavutia wanasheria na wanamazingira ambapo zaidi ya washiriki 250 kutoka zaidi ya nchi 25 wanatarajiwa kuhudhuria.