Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Korea ya Kaskazini kukabiliwa na uhaba wa nafaka:WFP/FAO

Korea ya Kaskazini kukabiliwa na uhaba wa nafaka:WFP/FAO

Karibu watu milioni tano nchini Korea kaskazini wataendelea kukabiliana na uhaba wa chakula hata baada ya taifa hilo kushuhudia ongezeko la mavuno.

Kufuatia uchunguzi uliondeshwa na ujumbe kutoka kwa shirika la chakula na kilimo duniani FAO kwa ushirikiano na shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP ni kuwa Korea kaskazini itahitaji kununua tani 867,000 za chakula mwaka 2010/2011.

(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)

Ujumbe huo hata hivyo ulipendekeza kutolewa kwa msaada wa tani 305,000 za chakula kwa watu wanaokabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula. Ujumbe huo ulizuru mikoa saba kati ya mikoa kumi nchini Korea kaskazini ambapo maghala yaliyotembelea hayakuwa na nafaka huku mahindi yaliyokuwepo kwa ugavi mwezi Oktoba kutoka kwa mavuno ya msimu uliopita hayakuwa salama kutumika kama chakula kufuatia njia duni za kuyahifadhi.

Wale ambao wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula ni pamoja na watoto, akina mama wajawazito wale wanaowalea watoto wachanga na watu wazee.