Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yazindua kalenda ya kilimo kwa Afrika

FAO yazindua kalenda ya kilimo kwa Afrika

Shirika la chakula na kilimo duniani FAO limezindua mfumo mpya wa kalenda kwa ajili ya nchi za Africa ambao utakuwa ukitoa mwongoza na maelekeo juu ya mazao yapi yanafaa kulimwa.

FAO inasema kalenda hiyo ya njia ya mtandao iliyozinduliwa na watalamu wake inajumuisha mazao zaidi ya 130 kuanzia maharagwe, maduriani, ngano hadi matikitimaji. Inawalenga wahisani wote, mashirika, serikali, wafanyakazi na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na wakulima barani Afrika. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Mfumo huo unaojulikana kwa jina la kalenda yenye kumbukumbu ya haraka,unajumuisha nchi 43 za afrika ambao utakuwa na kazi moja ya kutoa ushauru mazao yapi yalimwe na wakati gani yanapaswa kwa kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa.

Kalenda hiyo mpya inatajwa kuwa ni njia mjalabu ya kukabiliana na dharura inayoweza kujitokeza hasa wakati wa ukame ama wakati wa mafuriko.

Mmoja wa wakurugenzi wa FAO Shivaji Pandey amesema kuwa suala la kupatikana mbegu bora ni changamoto kubwa ambayo inapaswa kutatuliwa kwa kuzingatia matatozo ya ukosefu wa chakula na wakati huo huo kuwa makini na suala la mabadiliko ya tabia nchi.