Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UM na Rais wa Somaliland wajadili usalama

Mwakilishi wa UM na Rais wa Somaliland wajadili usalama

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia na ujumbe wake wamefanya mazungumzo na Rais wa Somaliland Ahmed Mohamed Mohamed Silanyo.

Balozi Augustine Mahiga na ujumbe wa watu wane ambao wamezuru jimbo la Puntland kwa mara ya kwanza wamejadili na Rais Mohamed Silanyo masuala ya amani, usalama na maendeleo. Jayson Nyakundi anaarifu.(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)

Waziri wa mashauri ya kigeni wa eneo lililojitenga kutoka Somalia la Puntland amesema kuwa mazungumzo kati ya rais Silanyo na balozi mahiga yalilenga zaidi masuala ya maendeleo na amani ya nchi. Amesema kuwa mwakilishi huyo wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa atakuwa katika eneo la Somaliland kwa muda wa siku mbili na atafanya mikutano na maafisa wengine wa utawala wa Somaliland akiongeza kuwa ziara hiyo ni sehemu moja ya juhudi za jamii ya kimataifa ya kuunga mkono uongozi wa rais Silanyo.

Akifanya ziara ya ghafla katika jimbo la Puntland siku ya Jumatano balozi Mahiga aliupongeza utawala wa jimbo hilo kwa juhudi zao za kupambana na magaidi ambapo pia alifanya mkutano na rais wa jimbo hilo Abdurrahman Mohammed Farole.