Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ajadili malengo ya milenia na rais wa Uchina

Ban ajadili malengo ya milenia na rais wa Uchina

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye yuko ziarani nchini Uchina na leo mjini Beijing amekutana na Rais wa nchi hiyo Hu Jintao.

Ban na mwenyeji wake wamejadili masuala mbalimbali yakiwemo mabadiliko ya hali ya hewa, malengo ya maendeleo ya milenia, masuala ya Korea na Afrika. Ban amesema ana imani Uchina inaweza kuwa na jukumu muhimu katika masuala ya ulinzi wa amani na kutafuta suluhu ya kisiasa katika migogoro barani Afrika ikiwemo Somalia na Sudan.

Naye Rais Jintao ameelezea kuwa Uchina inaunga mkono kwa dhati juhudi za Umoja wa Mataifa na hususan za Katibu mkuu Ban Ki-moon katika kutafuta suluhu ya amani, mabadiliko ya hali ya hewa na malengo ya maendeleo ya milenia.