Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IFRC yaomba msaada kwa ajili ya waathirika wa typhoon Ufilipino

IFRC yaomba msaada kwa ajili ya waathirika wa typhoon Ufilipino

Athari za uharibifu uliosababishwa na kimbuga Megi baada yam vu za typhoon nchini Ufilipino zinaendelea kujitokeza na shirikisho la la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu IFRC limetoa ombi la kimataifa la msaada wa dola milioni 4.3.

Fedha hizo zitasaidia katika shughuli zinazoendelea za uokozi na ujenzi mpya zinazoendeshwa na shirika la msalaba mwekundi nchini Ufilipino kwa kuwasaidia maelfu ya waathirika tangu kimbunga kulikumba eneo la kaskazini mwa nchi hiyo jana Jumatatu na kukatili maisha ya watu 31 na kusababisha uharibifu mkubwa katika mikoa mine ya jimbo hilo la kaskazini.

Inakadiriwa kwamba familia 427,300 ambazo ni takribani watu milioni mbili wameathirika na typhoon huku watu elfu nane wakipata hifadhi katika vituo maalumu 22, nyumba 31,000 zimebomolewa na nyingine 118,000 zimeharibika kiasi. Tathimini ya awali imebaini kuwa msaada wa haraka wa chakula, maji safi ya kunywa, malazi na madawa unahitajika.