Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mogwanja kuwa naibu mkurugenzi mkuu mpya wa UNICEF

Mogwanja kuwa naibu mkurugenzi mkuu mpya wa UNICEF

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Martin Mogwanja kuwa mmoja wa manaibu wakurugenzi wakuu watatu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Mogwanja atachukua nafasi ya Omar Abdi ambaye anashika wadhifa mwingine katika shirika hilo.

Mogwanja ambaye ni raia wa Kenya hivi sasa ni mwakilishi wa UNICEF nchini Pakistan na mwaka 2009 aliteuliwa kuwa mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini humo.

Kufuatia kutangazwa kwa uteuzi huo mkurugenzi mkuu wa UNICEF Anthony Lake amesema amefurahishwa na utezi huo wa bwana Mogwanja. Mogwanja alijiunga na UNICEF mwaka 1977 na amefanya kazi kama mwakilishi wa shirika hilo nchini Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na pia kama naibu mkurugenzi wa kanda ya afrika Magharibi na Afrika ya kati wa shirika hilo.

Ana ujuzi mkubwa katika masuala ya mipango, uratibu na utekelezazi wa programu mbalimbali za UNICEF katika kuboresha maisha ya wanawake na watoto.