Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

A.Magharibi inajitahidi kushirikisha wanawake katika amani:Djinnit

A.Magharibi inajitahidi kushirikisha wanawake katika amani:Djinnit

Kitendo cha wanawake kubakwa kwenye maandamano ya amani mjini Conakry nchini Guinea mwezi septemba mwaka jana kimeonyesha hali inayowakabili wanawake Afrika ya Magharibi kwa mujibu wa mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika kanda hiyo.

Bwana Said Djinnit ametoa kauli hiyo hii leo wakati wa kuadhimisha mwaka wa 10 wa azimio namba 1325 la baraza la uslama linalotoa wito wa kuwahusisha wanawake katika mipango ya amani na ujenzi mpya baada ya vita. Bwana Djinnit pia amekumbusha azimio lililoridhiwa na nchi za Afrika ya Magharibi mjini Dakar Senegal liitwalo "Women Count for Peace." Kwamba wanawake waastahili katika masuala ya amani.

Amesema tukio la Septemba 2009 limeonyesha jinsi wanawake walivyo katika hali ya hofu Afrika ya Magharibi na hivyo juhudi zinahitajika mara mbili kutekeleza azimio namba 1325 linalotokana na kongamano la Dakar ambako wananchi wanachama waliwakilishwa ikiwemo Guinea na wakaahidi kuwa na mipango ya kitaifa kufuatilia utekelezaji wa azimio hilo.