Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanasoka barani Ulaya wajitosa kukabiliana na njaa

Wanasoka barani Ulaya wajitosa kukabiliana na njaa

Kundi kubwa aa wanamichezo wa soka, barani Ulaya mwishoni mwa juma watakuwa viwanjani kwa sababu kuu moja tu ya kutoa mwito kwa serikali mbalimbali kuhakikisha kwamba zinatoa kipaumbele cha kutokomeza njaa duniani.

Kundi hilo linajumuisha wachezaji, makocha, pamoja na waamuzi 292 wanatazamiwa kuwashawishi zaidi ya watazamaji milioni 146 watakaomiminika viwanjani ili waunge mkono azimio la Umoja wa Mataifa linalotaka kuwepo kwa shinikizo kwa viongozi wa dunia kuanza kutekeleza mipango ya kutokomeza njaa. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kampeni hiyo iliyopewa jina la puliza kipyenga cha manjano inataka kuleta uamusho wa kukabiliana na tatizo la njaa ambalo hadi sasa limewakumba zaidi ya watu milioni 925 duniani kote.

(SAUTI YA JAQUES  DIOUF)

Tukio hilo linatazamiwa kupambwa na wanamichezo mbalimbali mashuhuri ambao wataingia dimbani huku wakiwa wamevalia fulana zenye ujumbe usemao puliza kipyenga cha manjano ili kukoa maisha ya malioni ya watu duniani kote.

Wachezaji kama mshindi wa kiatu cha dhahabu kwenye kombe la dunia Diego Forlan, Lionel Messi wanatazamia kuwa mstari wa mbele.