Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Changamoto za dunia ni kubwa, lazima tuungane-Ban

Changamoto za dunia ni kubwa, lazima tuungane-Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa kwa wakati huu hakuna taifa linaloweza kujitapa kuwa lipo salama kuzikwepa changamoto za dunia pasipo kutegemea upande mwingine.

Bwana Ban ameuambia mkutano wa kimataifa uliofanyika Marrakesh, Morocco kuwa katika historia ya dunia, hakuna wakati mgumu unaokabiliwa na changamoto mbalimbali kama unavyoshuhudiwa sasa, hivyo lazima mataifa yaungane kusaka ufumbuzi wa changamoto hizo kwa pamoja.

Amehimza haja ya kukusanya nguvu ya pamoja na kuzitatua changamoto hizo ambazo amesema haziizingatii mipaka wala uwezo wa dola moja.

Bwana Ban ambaye alikuwa akuzungumza kwenye kongamano la kimataifa lililojadilia siasa za kimataifa amesema kuwa Umoja wa Mataifa licha ya kuwa chombo kinachopeleka ushawishi wake duniani kote, lakini hata hivyo hakiwezi kufanya kazi peke yake pasipo kutegemea uungwaji mkono toka kwa nchi wanachama.