Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kunawa mikono kwa sabuni ni muhimu kwa afya:UM

Kunawa mikono kwa sabuni ni muhimu kwa afya:UM

Watu zaidi ya milioni 200 duniani kote, kuanzia ngazi ya familia, viongozi wa serikali, wanafunzi na hata watu mashuhuri kesho ijumaa wanaadhimisha siku ya kunawa mikono kwa sabuni.

Siku hii inaadhimishwa kila October 15, na mkazo unaozingatiwa ni kuhimiza wananchi kuwa na tabia ya kunawa mikono kama sehemu ya kuweka katika mazingira mazuri afya zao. Inadaiwa kwamba magonjwa ya mripuko ikiwemo kipindupindu ni madhara yanayotokana na kukosekana kwa mwamko huo wa unawaji mikono. Zaidi ya watoto milioni 3.5 waliochini ya umri wa miaka 5 hupoteza maisha kila mwaka.

Hali ni mbaya zaidi katika eneo la Mashariki na Kusin mwa Afrika ambako takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya watoto 250,000 hufariki dunia kila mwaka kuto kana na kuugua kipindupindu.