UM, AU pamoja na OECD watoa ripoti ya pamoja kuhusu uchumi wa Afrika

UM, AU pamoja na OECD watoa ripoti ya pamoja kuhusu uchumi wa Afrika

Mashirika yakiwemo afisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na ushauri kuhusu bara la Afrika UN-OSAA lile la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo pamoja na lile la maendeleo ya bara la Afrika AU-NPCA yanatarajiwa kutoa ripoti inayopendekeza kupanuliwa kwa uchumi wa nchi za Afrika.

Kulinga na utafiti uliofanya wenye kauli mbinu "upanuzi wa uchumi barani Afrika" ni kuwa hali hiyo itapunguza kutegemea mali asili tu kwa nchi nyingi za Afrika kwa uchumi wao na kupanua mapato yao kutoa pande zingine kama mawasilino , kilimo na utalii. Mkurugenzi mkuu wa AU-NPCA Ibrahim Assane Mayaki anasema kuwa ripoti hii inaangazia vile bara la Afrika linaweza kuporesha uchumi wake na maendeleo na pia kuonyesha vile bara la Afrika limechangia kukua kwa uchumi duniani.