Skip to main content

Viongozi wa Afrika wakutana mjini Addis Ababa kujadili changamoto za kimaendeleo barani

Viongozi wa Afrika wakutana mjini Addis Ababa kujadili changamoto za kimaendeleo barani

Mamia ya mawaziri kutoka nchi mbali mbali barani Afrika , wataalamu wa maendeleo na makundi kadha kutoka Afrika wanakutana mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa kwenye kongamano la saba kuhusu maendeleo barani Afrika.

Kati ya masuala yatakayojadiliwa kwenye kongamano hilo ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa na usalama na pia mabadiliko ya hali ya hewa na afya ya watu , jinsi na vijana. Kongamano hilo linafunguliwa rasmi kesho jumanne lakini hata hivyo vikao vya mapema tayari vimeanza kuandaliwa vikiwemo vya kujadili maendeleo ya vijijini ambapo asilimia 70 ya watu barani afrika wanaishi. Ben Malor wa radio ya Umoja wa mataifa alipata kuzungumza na Stephen Muchiri kiongozi wa shirikisho la wakulima kutoka afrika mashariki

(SAUTI YA STEPHEN MUCHIRI)

Kongamano hilo linaandaliwa kupitia ushirikiano wa benki yamaendeleo barani Afrika , tume ya Umoja wa Mataifa barani afrika na muungano wa Afrika kujadili changamoto zinazokabili maendeleo barani Afrika.