Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mcheza kambumbu mashuhuru wa kike aingia kwenye orodha ya mabalozi wema wa UM

Mcheza kambumbu mashuhuru wa kike aingia kwenye orodha ya mabalozi wema wa UM

Mcheza kandada wa kike mashuhuri duniani ambaye ni raia wa Brazil Marta Vieira da Silva ameteuliwa na shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP kama mtetesi wa masula ya wanawake ikiwa ni moja ya njia ya kupambana na umaskini duniani.

Bi Vieira da silva ambaye anachezea klabu ya FC Gold Pride nchini Marekani aliibuka mshindi wa tuzo la FIFA la mcheza kandada bora zaidi wa kike duniani kwa miaka minne mfululizo toka mwaka 2006 hadi 2009. Mcheza kandanda huyo anatajwa kuwa mfano mzuri wa akina mama na wasichana kote duniani na ambaye anawapa moyo wa kucheza kandada na huenda akawawezesha baadhi yao kuja pamoja kutimiza malengo ya milenia. Baada ya kuteuliwa kuwa balozi mwema wa Umoja wa mataifa mjini Stockholm mcheza kandanda huyo alisema kuwa atafanya juhudi za kutimizwa kwa vita dhidi ya umaskini itimiapo mwaka 2015. Kati ya wacheza kandada kwenye orodha hiyo ni pamoja na Ronaldo, zinedina zinade na Didier Drogba.