Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupambana na njaa duniani ndiyo ajenda kuu kwenye mkutano wa UM mjini Rome

Kupambana na njaa duniani ndiyo ajenda kuu kwenye mkutano wa UM mjini Rome

Kamati inayohusika na usalama wa chakula duniani CFS inaandaa mkutano wake wa kila mwaka kwenye makao ya shirika la chakula na mazao duniani FAO mjini Rome huku ikikabiliwa na changamoto kushughulikia maswala tata yakiwemo unyakuzi wa ardhi na uvumi kuhusu bidhaa za kilimo.

Kamati hiyo inashugulikia masuala kadha yakiwemo ya chanzo cha njaa na utapia mlo. Mkutano huo unaandaliwa baada kuongezeka kwa bei ya chakula duniani ambayo ni changamoto kubwa kwa usalama wa chakula duniani. Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani FAO Jacques Diouf anasema kuwa kiasi cha watu walio na njaa duniani ni kikubwa kuliko cha mwaka 1996.

(SAUTI YA DIOUF)

Naye mwakilishi maalumu wa UM kuhusu haki ya kuwa na chakula Olivier de Schutter anayehudhuria mkutano huo amesema kuwa mkutano huo utakuwa ni kama mtihani wa kamati ya CFS wa kushughulika masuala tata kama vile ya unyakuzi wa ardhi na uvumi kuhusu bidhaa za kilimo.