Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfuko wa kimataifa wa fedha bado unayumba:IMF

Mfuko wa kimataifa wa fedha bado unayumba:IMF

Shirika la fedha duniani IMF limesema hatua za kukwamua tena uchumi wa dunia zimepata pigo kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa jana mjini Washington.

Ripoti hiyo ya mtazamo wa fedha inaonyesha kwamba masoko ya fedha bado yanatiwa hofu na kiwango kikubwa cha madeni ya sekta za umma na samani zinadhohodhiwa na benki mbalimbali duniani.

Kwa mujibu wa Jose Vinals mtaalamu wa masuala ya fedha wa IMF mfumo wa fedha bado unayumbishwa na uchumi wa dunia, kwa sababu kuna masuala mawili yanayohitaji kushughulikiwa nayo ni madeni makubwa ya umma katika nchi nyingi zilizoendelea na mfumo wa benki ambao kwa nchi nyingi bado haujasimama imara kutokana na mdororo wa uchumi.

Hata hivyo amesema uchumi wa dunia umeenza kuimarika , lakini mtazamo wa fedha wa kimataifa bado haujatengamaa na unakabiliwa na hatari tena. Amesema ingawa kujiamini kumeanza katika baadhi ya nchi hasa barani Ulaya bado kujiamini huko hakujakamilika, hivyo matatizo ya madeni na kuyumba kwa setka ya benki kukishughulikiwa ipasavyo hali itatengamaa.