Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa baraza la usalama kuzuru nchini Uganda na Sudan

Ujumbe wa baraza la usalama kuzuru nchini Uganda na Sudan

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili masuala yatakayomulikwa katika mwezi huu wa Oktoba ambapo Uganda ndiye Rais wa baraza hilo.

Balozi wa Uganda kwenye Umoja wa Mataifa Ruhaganda Rugunda akizungumza na idhaa hii amesema kwa mwezi mzima vikao vya baraza la usalama vitaghubikwa na masuala ya afrika.

(SAUTI YA RUHAKANA RUGUNDA)

Rugunda ambaye ataongoza vikao vyote vya baraza la usalama kwa mwezi huu amesema suala la kura ya maoni ya Sudan litasalia kwa muda kwenye baraza hilo ikiwa na mambo ningine ya Afrika kwa sababu ni bara linalozongwa na matatizo mengi

(SAUTI RUHAKANA RUGUNDA)