Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Helkopya ya UM iliyo na misaada imepata ajali Pakistan

Helkopya ya UM iliyo na misaada imepata ajali Pakistan

Helkopta inayotumiwa na shirika la mpango wa chakula duniani WFP kusafirisha msaada kwa waathirika wa mafuriko Pakistan imelazimika kutua kwa dharura kwenye jimbo la Sindh nchini humo.

Kwa mujibu wa WFP tukio hilo lilijiri wakati wakiwa katika mpango wa kuwasilisha msaada wa biskuti kwa waathirika wa mafuriko. Msemaji wa WFP Emilia Casella amesema hakuna aliyekufa wakati helkopta hiyo ilipolazimika kutua na ilikuwa na abiria 12.

Amesema kuna kituo cha jeshi la Pakistan karibu na palipotokea ajali hiyo na hivyo wanajeshi walisaidia kuokoa abiria na kuwapeleka majeruhi hospitali. Kulikuwa na wafanyakazi wa ndege waane wa Urusi, wanne wa Pakistan na abia wawili wa Australia na Msudan mmoja. Wizara inayohusika na masuala ya anga ya Pakistan imearifiwa na inafanya uchunguzi wa ajali hiyo.