Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu lasisitiza haki ya maji na usafi

Baraza la haki za binadamu lasisitiza haki ya maji na usafi

Baraza la haki za binadamu limesisitiza kwamba haki ya maji na usafi inatoka kwenye haki ya viwango bora vya maisha ambayo iko katika mikataba mingi ya kimataifa ya haki za binadamu.

Akizungumza katika mkutano wa baraza hilo mjini Geneva Catarina de Albuqueque ambaye ni mtaalamu wa binafsi wa wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu amesema hii inamaanisha kwamba haki ya maji na usafi imo katika mikataba ya haki za binadamu na hivyo ni suala la kisheria.

Ameongeza kuwa uamuzi huo muhimu utaweza kubadili maisha ya mamilioni ya watu ambao bado hawawezi kupata huduma ya maji safi na vyoo.