Mashirika ya UM yametaka suala la mamilioni ya wahamiaji wasio na vibali liangaliwe

30 Septemba 2010

Kundi linalohusika na masuala ya uhamiaji duniani GMC limesema wahamiaji wengi wananyimwa haki zao na kukabiliwa na changamoto kubwa sehemu mbalimbali duniani.

Kundi hilo linasema kwa sasa kuna mamilioni ya wahamiaji wasiokuwa na vibali halali duniani kote jambo ambalo linawafanya wahamiaji wengine kutengwa na kupitia mateso mengi ikiwemo kuzuiliwa kwa muda mrefu au hata kufanywa watumwa wakati mwingine, kubakwa na hata kuuawa. Jayson Nyakundi na ripoti kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

GMG pia limesema kuwa wahamiaji wa kike wanakabiliwa na hatari nyingi zikiwemo dhuluma za kijinsia , kuambukizwa maradhi ya ukimwi na kunyimwa afya ya uzazi. Limeongeza kuwa mara nyingi watoto wa wahamiaji hupigwa marufuku kuhudhuria masomo au kunyimwa haki muhimu hata kama wazazi wao wanachamgia kukua kwa uchumi wa nchi wanazoishi.

Linasema wengi wa wahamiaji hawa huanguka mikononi mwa walanguzi wa binadamu huku watoto wasio na wakubwa wao wakiwa kwenye hatari zaidi. Navi Pillay ni mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa

(SAUTI YA NAVI PILLAY)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter