Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jopo la haki za binadamu kusikia ushahidi wa waathirika wa ubakaji DR Congo

Jopo la haki za binadamu kusikia ushahidi wa waathirika wa ubakaji DR Congo

Waathirika wa ubakaji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo watapata fursa ya kuzungumzia masahibu yao mbele ya jopo la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuanzia kesho huko Mashariki mwa nchi katika jimbo la Kivu ya Kusini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya kamishna wa haki za binadamu OHCHR, jopo hilo lililoambatana na naibu kamishna wa haki za binadamu na ushirikiano wa serikali ya Congo litawasikiliza waathirika na wengine juu ya waliyoyapitia , maoni kuhusu njia za kisheria, tiba, na hatua za kuwarejesha katika maisha ya kawaida ikiwepo ushauri nasaha na msaada wa kiuchumi uliopo. Navi Pillay ni Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa

(SAUTI YA NAVI PILLAY)

Mpango huo mbali ya kuongozwa na ofisi ya kamishna wa haki za binadamu unasaidiwa na hospitali ya Panzi na ofisi ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO. Mpango huo utaanza rasmi kazi ya kuzungumza na waathirika hao kesho Septemba 30 mjini Bukavu Kivu ya Kusini na kisha kusafiri katika majimbo mengine hadi Oktoba 10 na watafanya kongamano Oktoba 12 mjini Kinshasa kujadili yale waliyoshuhudia na kusikia na wadau mbalimbali wakiwemo serikali ya Kinshasa, Umoja wa Mataifa, jumuiya ya kimataifa na jumuiya za kijamii.