Skip to main content

UM wahofia mfumo wa sheria nchini Cambodia

UM wahofia mfumo wa sheria nchini Cambodia

Mwakilishi maalumu wa wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Cambodia Surya P. Subedi amesema kumekuwepo na matumizi mabaya ya sheria dhidi ya kuchafuliana majina na taarifa potofu nchini humo.

Akiwasilisha ripoti yake kwenye kikao cha 15 cha baraza la haki za binadamu mjini Geneva hii leo amesema ingawa Cambodia imepiga hatua kubwa katika miaka kadhaa iliyopita katika kuimarisha haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kufanyia marekebisho baadhi ya sheria muhimu lakini bado kuta matatizo.

Subedi amesema nchi hiyo inaghubikwa na matatizo mengi ya kisheria ikiwemo kulinda na kuchagiza haki za binadamu hasa kwa sababu demokrasia bado haijamea mizizi nchini humo. Amesema maeneo ambayo bado yanatia mashaka ni umiliki wa ardhi na haki za nyumba, uhuru wa kujieleza na changamoto za mfumo wa sheria.