Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kura ya maoni Sudan itakuwa huru na ya haki: Taha

Kura ya maoni Sudan itakuwa huru na ya haki: Taha

Makamu wa rais nchini sudan Ali Osman Mohamed Taha amesema kuwa watu wa kusini mwa Sudan watapiga kura kwa njia huru na yenye uwazi mwezi Januari mwaka ujao wakati watakapoamua ikiwa watajitenga na eneo la kaskazini au watabaki kuwa wananchi wa nchi moja , kulingana na makubalino ya mani ya CPA yaliyomaliza vita kati ya serikali ya kaskazini mwa Sudan na jeshi la SPLM lililo kusini.

Akihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa Taha amesema kuwa wenyeji wa kusini mwa sudan wataruhusiwa kutekeleza haki yao pila kuingiliwa kati.Wakati huo pia wenyeji wa eneo la kati mwa Sudan la Abyei nao watapiga kura kando kuamua iwapo watasalia kuwa kaskazini au watajiunga na kusini.

Kwenye mkutano kuhusu Sudan ulioitishwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon kando na mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York , viongozi wa dunia waliunga mkono mikakati hiyo ya pande zote mbili nchi Sudan ya kutekeleza makubalino ya CPA.

Taha pia amesema kuwa serikali ya Sudan inafanya juhudi za kuhakikisha kuwepo kwa amani keenye jimbo la Darfur ambalo limekumbwa na mzozo tangu mwaka 2003 na kuleta uwiano kati ya jamii zinazoishi kwenye jimbo hilo.