Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kura ya maoni Sudan ni muhimu sana: Mkapa

Kura ya maoni Sudan ni muhimu sana: Mkapa

Mkuu wa jopo maaluum lililoteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kuangalia kura ya maoni nchini Sudan anasema kura hiyo ni kipimo cha hatma ya mamilioni ya raia wan chi hiyo.

Benjamini Mkapa aliyekuwa Rais wa zamani wa Tanzania anaongoza jopo la watu watatu waliopewa jukumu la kuangalia kura hiyo ya maoni inayotarajiwa kufanyika Januari 9 2011. Kura hiyo itaamua endapo Sudani Kusini ijitenge na kuwa taifa huru ama la.

Akizungumza na Idhaa hii kando na mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Bwana Mkapa amefafanua jukumu lao.

(SAUTI BENJAMIN MKAPA)