Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa DR Congo waiomba Tanzania kuchelewa kuwarejesha nyumbani

Wakimbizi wa DR Congo waiomba Tanzania kuchelewa kuwarejesha nyumbani

Wakimbizi toka Jamhuri ya Kidemocracy Congo waliko kwenye makambi ya Nyarugusu Mkoani Kigoma Tanzania ,wameimba serikali ya Tanzania kutoanza kutekeleza mpango wa kuwarejeshwa makwao kama ilivyo fanya kwa wakimbizi wa Burundi waliokuwa wakihifadhiwa kwenye kambi ya Mtabila ambayo pia ipo mkoni humo Kigoma.

Wakimbizi hao wanapatiwa msaada na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania. Hivi sasa serikali imekuwa ikiwaomba wakimbizi hao wa Congo kuanza kurejea nyumbani lakini kwa hiari yao wenyewe.

Wakimbi hao wa Congo wametoa rai hiyo baada ya kuhudhuria bunge la vijana wa wakimbizi lililoandaliwa na UNHCR  kwa ushirikiano na UNFPA katika kambi ya Nyarugusu. bunge hilo linajadili changamoto mbalimbali zinazowakabili viajana wakimbizi. Mwandishi wetu George Njogopa ametembelea kambi hiyo ya Nyarugusu Mkoani Kigoma na kutuandali taarifa ifuatayo.