Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Papua New Guinea kuchangia wanajeshi wa kulinda amani kwa UM

Papua New Guinea kuchangia wanajeshi wa kulinda amani kwa UM

Waziri mkuu wa Papua New Guinea amesema kuwa nchi yake inakaribia kuchangia wanajeshi kwa hatakati za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.

Akilihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa Michael Somare amesema kuwa ulimwengu sio salama tena kuliko wakati Umoja wa Mataifa ulipobuniwa akitoa mfano wa Iraq , Korea na mashariki ya kati. Bwana Somare amesema kuwa mizozo ya kidini na ya kijamii inaendela kushamiri katika sehemu nyingi za afrika , Amerika ya kusini na sehemu za mashariki mwa ulaya na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua kutatua masuala haya.

Somare amesema kuwa serikali ya nchi yake imepitisha musuada wa kimataifa unaoruhusu Papua New Guinea kushiriki kwenye oparesheni za umoja wa mataifa za kulinda amani. Pia ametoa wito wa hatua kuchukuliwa kukabiliana na ugaidi na kuEndelea kuongezeka kwa zana za kinyuklia.