Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa kimataifa uongezwe kuleta amani:Pinda

Msaada wa kimataifa uongezwe kuleta amani:Pinda

Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuongeza msaada wa kusaidia katika juhudi za kuleta mani.

Akizungumza kwenye mjadala wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa hii leo hapa New York bwana Pinda amesema Afrika imekuwa msitari wa mbele kujaribu kutatua matatizo hasa ya vita yanayolikumba bara hilo kama vile Somalia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan.

Amesema hata hivyo tatizo kubwa ni fedha zinazosababisha shughuli hiyo kutofanikiwa ipasavyo akitolea mfano vikosi vya pamoja vya kulinda amani Darfur vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID na vile vya muungano wa Afrika Somalia AMISOM.

Pinda ambye katika hotuba yake amezungumzia pia msimamo wa Tanzania kuunga mkono Palestina kuwa na taifa lao kuishi sambamba na Israel ameungana na viongozi wengine wa Afrika kutaka baraza la usalama litoe nafari ya kudumu kwa bara la Afrika.

(SAUTI MIZENGO PINDA)