Leo inasherehekewa siku ya kimataifa ya utalii
Leo ni siku ya kimataifa ya utalii, ambayo mwaka huu inaadhimishwa kwa kauli mbiu utalii na bayo-anuai.
Katika ujumbe maalumu wa kuadhimisha siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema utalii na masuala ya bayo-anuai vinakwenda sambamba na haviwezi kutenganishwa. Amesema mwaka huu ambao ni mwaka wa bayo-anuai unatoa fursa muafaka ya kujikita katika juhudi za haraka za kulinda bayo-anuai kwa ajili ya utajiri, afya na maslahi ya watu katika nchi zote duniani.
Ban pia ameipongeza sekta ya utalii duniani kwa kutambua umuhuimu wa kulinda bayo-anuai na ametoa wito kwa pande zote kuimarisha jukumu lao la kuendeleza ulinzi huo.