Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika ipewe nafasi na vikwazo viondolewe:Mugabe

Afrika ipewe nafasi na vikwazo viondolewe:Mugabe

Mtazamo wa kutaka nafasi ya Afrika kwenye baraza la usalama umeungwa mkono pia na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Rais Abdulaye Wade wa Senegal, waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi, Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan na Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye pia amelaani matumizi ya vikwazo vya kiuchumi na hatua zingine hasa katika uhusiano wa kimataifa.

Amesema matumizi ya vikwazo yanakwenda kinyume na misingi ya ushirikiano wa kimataifa iliyopo kwenye mkataba wa Umoja wa Mataifa na vinatoa adha kubwa kwa mamilioni ya watu wasio na hatia.

(SAUTI ROBERT MUGABE)

Viongozi wengine wa afrika wanaounga mkono mabadiliko kwenye Umoja wa Mataifa na baraza la usalama na hasa afrika kupewa nafasi zaidi ni Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, Rais wa Kenya Mwai Kibaki na mwakilishi wa Burundi na Rais Yoweri Museveni wa Uganda.