Rais wa Somalia ataka jumuiya ya kimataifa kuisaidia kukabiliana na ugaidi wa al-Shabaab

Rais wa Somalia ataka jumuiya ya kimataifa kuisaidia kukabiliana na ugaidi wa al-Shabaab

Mjadala wa kila mwaka wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa umeendelea leo Jumamosi kwenye makao makuu hapa New York.

Mjadala huo unaoendelea hadi Septemba 30 ili kuhakikisha viongozi na wakuu wa nchi zaidi ya 130 wanapata fursa ya kutoa mawazo yao kuhusu masuala mbalimbali yanayoisumbua dunia. Mada kuu ya leo ni kuimarisha jukumu la Umoja wa Mataifa katika utawala wa dunia.

Hadi sasa zaidi ya marais 60, mawaziri wakuu na wawakilishi wengine wamewasilisha maelezo na mitazamo yao katika mjadala huo kuhusu mada mbalimbali zikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa, upokonyaji wa silaha za nyuklia, amani na usalama na kutaka mabadiliko kwenye Umoja wa Mataifa.

Miongoni mwa waliozungumza hii leo ni Rais wa Somalia Sheikh Sharifu Ahmed aliyeutaka Umoja wa Mataifa kuendelea kusaidia kwa kila hali kurejesha amani nchini mwake hasa kutoikana na hofu ya ugaidi kutoka kundi la Al-Shabaabu, Izbollah islam, na makundi mengine ya nje yanayosaidiwa na Al-Qaeida.

Wengine ni Rais wa utawala wa Palestina Mahmoud Abbas ambaye amesisitiza kuwa wataendelea kushirikiana na Umoja wa Mataifa kuhakikisha amani na utulivu uanapatikana mashariki ya Kati na kuona taifa la Palestina likiundwa. Naye mfalme Mswati II wa Swatzilandi ambaye hupanda na kutoka jukwaani kwa nderemo na vifijo

(SAUTI YA VIGELEGELE)

Amesema ufalme wa Eswatini unakubaliana na msimamo wa viongozi wengine wa Afrika wa kutaka mabadiliko kwenye Umoja wa Mataifa na hasa baraza la usalama ili Afrika iweze kupewa nafasi mbili za ujumbe wa kudumu na tano zisizo za kudumu,amesema anatumai mjadala huu wa baraza wa mwaka huu utapatia ufumbuzi suala hilo.