Baraza la usalama lajadili kusitisha vita na kuchagiza amani

Baraza la usalama lajadili kusitisha vita na kuchagiza amani

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limekutana jioni ya leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kujadili masuala ya upokonyaji silaha na kuchagiza amani.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni akizungumza katika mkutano huo amesema Afrika bado inakabiliwa na matatizo makubwa ya usalama na Umoja wa Mataifa unatakiwa kuzihusisha kwa karibu zaidi nchi hizo katika kuleta amani na utengamano.

(CLIP YOWERI MUSEVENI)

Naye waziri mkuu wa Uchina amesema nchi yake iko msitari wa mbele katika kulisaidia bara la Afrika kukomesha vita na kukumbatia amani kwa kuongeza msaada wa kufanikisha operesheni za amani, wa kiufundi, mafunzo na vifaa.