Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya kimataifa ya mabaharia na kazi zao

Leo ni siku ya kimataifa ya mabaharia na kazi zao

Leo ni siku ya kimataifa ya mabaharia ambayo imeadhimishwa kwa wito wa kutambua kazi ya mabaharia duniani.

Katibu Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya huduma za bahari ametoa wito kwa ulimwengu kutambua na kuthamini kazi muhimu inayofanywa na mabaharia duniani na kusaidia kuboresha mbinu za mazingira ya kazi zao. Jason Nyakundi na taarifa zaidi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani Efthimios Mitropoulos, katibu wa shirika la kimataifa la mabaharia IMO ametoa wito wa kutaka kutambuliwa kwa wafanyikazi hao ambao huduma zao mara nyingi hazitambuliwi.

Amesema kuwa kauli mbiu ya siku ya leo ikiwa "siku ya baharia" shirika la IMO lina nia ya kuwahakikishia mahabaria wanaofanya kazi ngumu kuwa wajibu wao unatambuliawa pamoja na maisha ya familia zao.  Bwana Mitropoulos amewataka wale wanaoshirika katika sekta ya huduma za baharini kuwahakikishia mazingira mema wafanyikazi wao na pia kuwapa malipo mazuri wafanyikazi wao.

Siku hii inaadhimishwa nyakati tofauti na sehemu mbali mbali dunini hasa san asana mapema mwezi Septemba inatumiwa kuangazia zaidi usalama wa sekta ya huduma za baharini na wajibu mkuu wa shirika la IMO.