Vijana wametakiwa kusaidia kuleta amani:Ban

Vijana wametakiwa kusaidia kuleta amani:Ban

Vijana wametakiwa kutoa mchango katika kuleta amani duniani, katika siku ambayo Umoja wa Mataifa unaadhimisha siku ya kimataifa ya amani.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye wiki iliyopita aligonga kengele ya amani mjini New York. Ban amesema mwezi huu wa Septemba unaashirika mwanzo wa mwaka wa kimataifa wa vijana ambao unajikita katika mambo mbalimbali yanayowahusu vijana.

Ban ametowa wito kwa dunia na kusema tujitahidi kuongeza juhudu kuwasaidia vijana, tuwape dunia ya amani na uvumilivu. Na kwa vijana wote jiungeni nasi, tusaidieni kufanya kazi ya kuleta amani, tupeni mawazo na mitazamo yenu, kuweni wabunifu na wenye ari, tusaidieni kupigania amani na maisha bora kwa wote.