Benki ya Dunia yaahidi kutoa zaidi ya dola billioni 1 kwa ajili ya kufanikisha malengo ya milenia

Benki ya Dunia yaahidi kutoa zaidi ya dola billioni 1 kwa ajili ya kufanikisha malengo ya milenia

Benki ya Dunia imeahidi kuongeza msuko wake kwa nchi zinazoendelea ili ziweze kufikia malengo ya maendeleo ya millenia.

Akizungumza kwenye Umoja wa Mataifa Rais wa Benki hiyo Robert Zoellick ameeleza kuwa Benki hiyo ya Dunia inakusudia kutoa kiasi kingine cha mabilioni ya dola kwa nchi hizo zinazoendelea ili ziweze kufukia malengo hayo kwa upande wa afya na elimu.

Amesema ili kufikia azma hiyo, benki hiyo iko tayari kutoa kiasi cha dola milioni 750 ambazo zitatumia kugharimia miradi ya uendelezwaji wa sekta za afya ya elimu. Kiasi hicho cha fedha kitapelekwa katika nchi zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara